Madereva wa teksi walalamikia kuathirika kwa biashara zao.

 

By Mercy Wangila

Kama kawaida, magari ya teksi ni aina ya magari yanayobeba idadi ya chini zaidi ya abiria.kufuatia kuenea kwa virusi vya Covid-19,sheria na masharti ziliwekwa kufuatwa na kila mmoja, hatua ambayo imechangia kudorora kwa biashara nyingi.

Matatu

 


-Madereva wa teksi eneobunge la Kanduyi katika Kaunti ya Bungoma, ni mojawapo wa wafanyabiashara ambao wameathirika pakubwa wakati huu ambao msambao wa Corona unaendelea kushuhudiwa nchini.                                                                                  —Vilevile wamehoji kutoweza kumudu kiasi cha fedha wanazotozwa kila kukicha kwa minajili ya kulipia mahali wanapoegesha magari hayo.

 

-Aidha, madereva hao wamedai kuhadaiwa mara kwa mara na maafisa wa polisi wakiwa katika harakati za kuendesha shughuli zao za kila siku.

 

-Fundi wa magari eneo hilo vilevile amedai kuathirika kutokana na kudorora kwa biashara za teksi.

 

-Mbali na hayo, wahudumu hao wameomba serikali kuingilia kati, kutetea haki ya vijana kiujumla kwa kuwapa ajira.