Wakaazi wa Bungoma waisuta serikali kwa kuongeza ushuru

0
60
picha inayoonyesha katikati mwamji wa Bungoma

By Victoria Magar

Wakaazi  wa kaunti ya Bungoma wameisuta serikali kwa kuongeza ushuru wa bidhaa muhimu wakisema hatua hiyo itafanya hali ya maisha kuwa ngumu zaidi.

Hali hii inajitokeza baaada ya bajeti mpya kusomwa mwezi uliopita,huku ikionekana dhahiri shairi kuwa bei ya bidhaa haswa bidhaa ya matumizi ya kila siku kwa maisha ya mwana nchi imeongezeka kwa aslimia kubwa sana.

picha inayoonyesha shughuli zinazoendelea katika mji wa Bungoma

Wakizungumza na idhaa hii wakaazi hao wakiongozwa na mwanamazingira Edward Kimakwa wamewanyoshea kidole cha lawama  wabunge kwa kutojali masilahi ya mwananchi wa kawaida na kuruhusu serikali kuongeza ushuru wa bidhaa muhimu kiholela.

Nao vijana wakiongozwa na Martin Simiyu wanasema licha ya hali ya maisha kuwa magumu wanasiasa wangali wanawalenga vijana na kuwatumia kwa manufaa yao ya kibinafsi wakisema ikiwa hali hiyo itaendelea hawatawapigia kura tena viongozi hao.

Aliongeza na kusema kuwa serikali inafaa kuangalia maslahi ya wananchi kwa sekta zote bila kuwanyanyasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here