Pigo Kwa Wafanyibiashara Wanaouza Kando Ya Barabara

0
206
wafanyibiashara kando ya barabara katika kaunti ya bungoma

By Raphael Situma

Serikali ilitangaza kuchukua hatua kwa wafanyibiashara wanaoendesha shughuli za uuzaji wa mboga na matunda kando ya barabara,sababu kuu ikiwa kuzuia maradhi mbalimbali yanayopatikana kando ya barabara ambapo kuna magari na watu wanaopita.

Amri hiyo kwa kiwango fulani imepokelewa kwa njia hasi kwa baadhi ya wafanyibiashara katika kaunti ya Bungoma.wengi wakidai kuwa hawajakaidi kukoma kuuza bidha zao kando ya barabara ilmradi serikali iwanjengee sehemu pa kuendeleza biashara zao,huku wakitoa madai kuwa sokoni kumejaa hivyo basi ni vigumu wao kufanya biashara sehemu hiyo kutokana na mkurupuko wa Covid 19.
picha ya wafanyibiashara kando ya barabara bungoma
Wilkister Nekesa,muuzaji matunda katika soko la Chebukube ameeleza kuwa kuuza kando ya barabara kuna faida,watu wengi hawana muda wa  kuingia sokoni kununua bidhaa,ikizingatiwa kuwa mtu huwa na haraka  hivyo basi itamlazimu kuchukua bidhaa kando ya barabara haswa wakati huu ambapo kuna masharti ya kudhibiti msambao wa Korona.Bi. Nekesa ameirai serikali ya kaunti kuwa na huruma na kuwapanulia soko la Bungoma ili kufanyia shughuli za biashara kwa njia bora.
Linus Odhiambo,aliunga mkono kauli hiyo akieleza kuwa hakuna tofauti ya kuuza ndani ya soko na kando ya barabara huku akisisitiza kuwa pia kule ndani hali ya usafi sio nzuri. Fauka ya hayo,wanatozwa  ushuru sawa na wale wanaouza ndani ya soko. Aliomba serikali kudumisha usafi wa soko ndipo wauzaji waweze kufurahia mazingira bora.
Marufuku hayo ya  kuuza kando ya barabara ni sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha usalama wa mazao safi,haswa yanayouzwa kando ya barabara na barabara kuu.
Waziri wa Kilimo Bw. Peter Munya hapo awali alisema  wanunuzi  wametambua hatari za vyakula vichafu na wanadai vyakula  salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here