Wizara ya Afya Yahakikisha Ufikaji ya Chanjo ya Pili ya Astrazeneca

0
85
picha ya chanjo ya covid 19 zikiwasili nchini kenya
By Victoria Magar
Huku Zaidi ya watu elfu mia mbili wakiwa wamepokea chanjo kamili ya astrazeneka, idadi hiyo inakisiwa kuongezeka kufwatia kuwasili kwa chanjo hiyo siku ya jumatatu.
Wizara ya afya imesema kwamba hifadhi zote za mkoa humu nchini  zimepokea chanjo hiyo tayari kwa kupeana dozii ya pili ya chanjo hiyo.
Kulingana na mwenyekitu wa kusimamia chanjo ya korona daktari Willis Akhwale, chanjo hizo zilisambazwa kulingana na nambari zilizoko kwenye mfumo wa  chanjo ya wizara ya afya ,bohari la mkoa wa eldoret imepokea dozii 39000,kakamega ikapokea dozii elfu ishirini na nne, kisumu imepokea dozii elfu ishirini na nane na meru ika pokea dozii ya elfu kumi na mbili, mombasa imepokea dozi elfu kumi na tatu ,nairobi imepokea dozii elfu mia moja sabini na mbili na mia saba na nakuru imepokea dozii elfu thelathini na tisa.
picha ya chanjo ya covid 19 zikiwasili katika uwanja wa ndege.
Daktari Willis akhwale anafahamu kuwa usambazaji upya wa chanjo ambazo hazikutumika ilifanyika kwa wiki mbili zilizopita na baadhi ya kaunti ambazo ilishuhudia idadi ndongo ya watu wakupewa chanjo kama mandera,garissa na marsabit walirejesha chanjo hizo ilikuweza kusaidia kaunti jirani zilizokuwa na idadi kubwa, kaunti zingine pia katika ukanda wa ziwa victoria zilishuhudia idadi chache ya waliopokea chanjo kwa sababu ya kucheleweshwa kwa chanjo hiyo.
Kesi za virusi vya korona imekuwa ikiongezeka katika ukanda.wa.ziwa victoria huku mahospitali zikipitia wakati mgumu kwa sababu ya idadi ya wangonjwa, kulingana na rekodi za korona wiki moja iliyopita idadi ya walioambukizwa ni elfu mbili mia moja sabini na moja.
Idadi kubwa ya maambukizi ni kutoka kisumu  na watu mia nne hamsini na moja,siaya kaunti ikiwa na idadi ya mia nne arubaini na sita, busia ikirekodi idadi ya mia mbili sitini na tatu na homabay ikirekodi idadi ya mia mbili ishirini, ilhali kiwango cha maambukizi hapa nchini imesalia kuwa aslimia kumi huku watu thelathini wakifariki kuongeza idadi ya vifo vya korona kuwa elfu tatu mia tano kumi na nne.