Maoni ya Wakaazi wa Bungoma Kufuatia Amri ya Wizara ya Afya Kufunga Baadhi ya Kaunti

0
56
image of police officers in the street at curfew time
By Dishon Amanya
Vizuizi vya kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya korona katika mikoa ya Nyanza, Magharibi na baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa vimeibua hisia mseto kwa baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Bungoma.Amri hiyo ya ilitolewa na Wizara ya Afya baada ya maeneo hayo kurekodi asilimia sitini ya maambukizi ya msambao wa virusi vya Korona.
 
Wizara ya afya ilieleza kuwa ili kupunguza msambao zaidi,ililazimika kuweka vizuizi katika maeneo hatari, baada ya kufanya majadiliano na washikadau husika na baraza la Magavana.Maamuzi hayo yalipokelewa kwa hisia mseto kwa baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Bungoma.
 
CGN ilifanya mahojiano ya moja kwa moja na baadhi ya wafanyibiashara,wengi walionyesha kutoridhishwa na amri iliyotolewa na wizara ya afya.wengine wakimnyoshea kidole cha lawama kwa Rais wa Taifa,huku wakidai kuwa Rais ndiye aliyechangia katika msambao wa virusi hivi baada ya kuchangia umati katika kaunti ya Kisumu wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaraka.
 
Antonny Nderitu,Mfanyibiashara Bungoma alieleza,” Rais alikosea kuruhusu kusherehekea siku ya Madaraka Kisumu ambapo ilichangia kuleta umati wa watu,Siku hiyo angeamua iwe ya kimtandao kama ambavyo  yeye huhudhuria mikutano ya kimtandao akiwa pale Ikulu. vizuizi hivi sasa vimebadilisha hali ya maisha kwetu , kibinafsi sijazoea kurudi chumbani mapema.
image of police officers in the street at curfew time
 
Kulingana na kauli yake Nderitu,ni dhahiri shahiri kuwa maadhimisho ya siku ya Madraka Kisumu ilichangia katika msambao wa virusi vya Korona katika mikoa ya Magharibi na Nyanza.wakaazi walidokeza kuwa kila mara Rais anapozuru eneo fulani ni lazima umati uwe,masuala ya Uzinduzi wa Miradi ni suala ambalo Rais anaweza kuzindua tu akiwa Ikulu.
 
Kuwekwa kwa vizuizi vya “Curfew” na wizara ya afya imechangia katika kubadilika kwa utamaduni wa wakaazi wa mkoa wa magharibi, kama anavyoeleza mkaazi mmoja wa Bungoma Vincent Kegode.
 
Suala la kuweka vizuizi hasaa katika masula ya mazishi imebadilisha utamaduni wetu wa Waluhya.Ni kawaida yetu mwili kuchukua muda wa siku mbili kabla ya kuuzika, kwa sasa mambo ni tofauti utamaduni wetu umesahaulika.” Alieleza Kegode.
 
Mbali na hayo nafasi za kazi kwa wanaofanya kazi za mapishi katika sherehe zimepungua kwa sasa hawaruhusu umati katika sherehe hali ambayo imechangia watu wengi kutowatumia wapishi  hao kwa kuwa idadi ya wanaohudhuria mazishi au matanga imepunguzwa hadi hamsini.
 
Mbali na hayo wenyeji wanaelezea kuwa hali ya biashara sasa itapungua haswa kwa akina Mama Mboga ambao hutegemea mauzo yao wakati wa saa moja baada ya kufanya shughuli zingine wakati wa mchana,mida hiyo ndio wao huwa na nafasi ya kuendeleleza biashara yao baada ya kutoka kazini.
 
Wakaazi hao wanapendekeza serikali kufanya uhamasishaji zaidi dhidi ya janga la Korona,kuweka vizuizi hakuchangia katika kupungua kwa msambao wa virusi vya korona. Wanapendekeza kila Mkenya kujukumika kwa kuwa ni jukumu la kila Mkenya kuhakikisha kuwa yupo makini na afya yake.