Magoha Apiga Marufuku Matumizi ya Basi Za Shule

0
108
picha yake waziri wa elimu Magoha

By Tim Wandabwa

Hisia kinzani zinazidi kutolewa na wazazi pamoja na washikadau katika shule za  msingi na za upili kufwatia tangazo la waziri wa  elimu George Magoha  kupiga marufuku matumizi ya basi za shule kwa shughuli za kibinafsi ikiwemo hafla za mazishi na sherehe mbali mbali.

Hii ni baada ya mabasi ya shule kuonekana yakitumika kwenye shughuli na hafla mbalimbali ambazo haziendani na maswala ya shule.

picha yake waziri wa elimu Magoha akihutubia kwenye hafla

Wachache tuliozungumza nao katika mahojiano ya kipekee na kituo hiki wanasema si vyema kwa Magoha kupiga marufuku matumizi ya basi hizo kwa sababu mingi hununuliwa kupitia kwa halmashauri ya shule hizo almaarufu PTA ambao ni muungano wa walimu na wazazi.

Kadhalika pia wanasema waziri Magoha ajishughulishe na maswala muhimu katika sekta hiyo ya elimu na kuwachana na mambo yanayohusiana na matumizi ya mabasi ya shule kwa sababu ni jukumu la walimu wakuu japo sio jukumu la wizara ya elimu.

Pia wamesuta vikali walimu wakuu wanaotumia magari hayo  yaliyonunuliwa na serikal kama kitega uchumi kupitia hazina ya CDF wakisema pendekezo la Magoha lilifaa kutekelezwa tu kwa mabasi ya shule ambayo yalinunuliwa kupitia kwa hazina ya CDF.