Bi Catherine Wambilianga amwajiri mwanawe kama msaidizi wake

0
27
picha ya Catherine Wambilianga

By Tim Wandabwa

Wakenya wanazidi kumunyoshea kidole cha lawama mwakilishi wa kaunti ya Bungoma Bi Catherine Wambilianga kwa tuhuma za kumwajiri mwanawe Tessie Nakami kama msaidizi wake wa kibinafsi maarufu kama personal assistant kwa lugha ya kimombo na kumtengea mshahara wa Shillingi 363,000.

Kulingana na stakabadhi iliodhibitishwa na meza yetu ya habari,Nakami,ambaye ni mwanawe Bi Catherine Wambilianga anapata mshahara wa shilingi elfu mia tatu sitini na tatu na mia tano hamsini na tatu ikiwa ni kiwango cha juu  Zaidi ya msimamizi wa ofisi ya muwakilishi huyo wa kina mama hata katika nafasi ya kuwa tu msaidizi wa kibinafsi.

picha Catherine Wambilianga akizungumza katika mkutano

Kando na Tessie anayelipwa mshahara mkubwa kwa kuwa mwanawe Bi Wambilianga,kulingana na fomu ya malipo katika afisi ya mwakilishi huyo,meneja analipwa shilingi elfu hamsini na tano,katibu analipwa shilingi elfu hamsini na tano ,msaidizi mlinzi analipwa shilingi elfu ishirini,afisa wa mawasiliano analipwa shilingi elfu ishirini na tano na dereva analipwa shilingi elfu hamsini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here