Home Politics ODM na ANC kwenye Mvutano wa kuteuwa gavana Nyamira

ODM na ANC kwenye Mvutano wa kuteuwa gavana Nyamira

0
136
image of Amos Nyaribo

Mwandishi: Victoria Magar

Vuta nikuvute katika Kaunti ya Nyamira kuhusu uteuzi wa Naibu Gavana itaendelea kwa muda baada ya ODM kuendelea kushinikiza chaguo lake ndiye ateuliwe huku Gavana Amos Nyaribo akisisitiza kumteua James Gesami.

image of Amos Nyaribo

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, Jana alimtetea Gavana Nyaribo akikashifu ODM kwa kuhujumu uongozi wa Nyaribo kwa kumwekea vikwazo.

Amos Nyaribo

“Kama chama cha ANC tunapinga njama zinazoendelezwa na watu hao ambao wanataka kuvuruga uongozi wa Bw Nyaribo kwa kumsukumia kibarakala wao eti ndiye ateuliwe kama naibu wake,” Bw Mudavadi akasema kwenye mahojiano.

Kwa mara ya pili sasa, ODM imependekeza Bw Charles Rigoro ateuliwa chini ya kile ODM inasema ni mkataba uliokuwepo kwamba ODM na ANC walifaa kugawana uongozi wa Kaunti ya Nyamira kwa usawa.