Afueni kwa wafanyibiashara kaunti ya Bungoma

0
221

By Christine Musundi.

Wafanyibiashara katika kaunti ya Bungoma wamepata afueni baada ya shule kufunguliwa humu nchini.

Akizungumza mfanyibiashara wa duka la sare ya shule, ameeleza afueni ambayo ameweza kushuhudia ikilinganishwa na hapo awali ambapo shule zote zilikuwa zimefungwa kufuatia mkurupuko wa janga la korona.

Baadhi ya ahueni alizozipata, mojawapo ikiwa kuuza kwa sare kwa wingi,huku shule kadhaa zikifanya maagizo ya sare kulingana na idadi ya wanafunzi waliowasili shuleni.

Aidha changamoto anazokumbana nazo wakati huu wa shamrashamra za kurejea shuleni kwa wanafunzi ,wateja wengi hawajazingatia kanuni zilizowekwa na wizara ya afya haswa kuvalia barakoa vikamilifu ,kunawa mikono  na kusimama umbali wa mita moja

Vilevile wanafunzi wengine wamenenepa kupita kiasi na kuwalazimu wazazi kutafuta sare katika maduka mengine sababu ikiwa sare hizo haziwatoshi hivyo basi hisa zao zimebaki zimejalia.

Tawsira kamili imeshuhudiwa na wauzaji wa vitabu ikilinganishwa na hapo awali na sasa hivi.