Tamasha ya sanaa ya jinsia utamaduni vijana na michezo

0
257

By, Zepparine Mabele

Siku ya utamaduni ikiadhinishwa katika kaunti ya bungoma wadi ya sanga’alo mashariki  ambapo viongozi wa matabaka tofauti wamehudhuria ili vijana wapewe mafunzo na ushauri kutoka kwa watu wa nyadhifa mbalimbali.

Hafla hiyo ikiongozwa na waziri wa sanaa ya jinsia utamaduni vijana na michezo Bi. Everlyne Kakai amewataka wazazi pamoja na vijana kuwajibika ili kukomesha tabia zisizo murwa haswa wakati huu ambapo kuna janga la korona na wanapojipanga kurejea shuleni mwaka ujao.

Vilevile amesisitiza vijana kutilia maanani katika masomo yao na nidhamu kudumu siku zote ili kuepuka vikundi vibaya.

Kando na hayo ameongeza kuwa lengo lao kuandaa hafla hiyo ni kuwaleta pamoja vijana kutoka tabaka mbalimbali ili tu kuwaelimisha jinsi ya kujisaidia kimaisha wao wenyewe na kutangaza umoja ,ushirikiano na nidhamu.

Aidha naibu wa gavana charles ngome alitoa shukrani zake kwa wazazi kwa kuwaruhusu wana wao kuhudhuria hafla hiyo ili kupata mawaidha kutoka kwao kama viongozi wa kaunti ya Bungoma.

Hata hivyo alitoa ahadi yake kwa mangariba wote kuwapa sare kamili za utambulisho wao na kutenga fedha za kutengeneza mahali pao pa kupashia tohara na kufanya mafunzo kwa watoto wanaopashwa tohara.

Kwa kufanya hivyo kumekuwa njia mojawapo mwafaka wa kuunganisha vijana ili wajue  ni nini cha maana katika maisha yao ya badae.