Zahanati yapoteza shamba kwa mmiliki binafsi Trans Nzioa (video)

0
693

Bodi simamizi katika zahanati ya Maridadi eneo bunge la kwanza], kaunti ya Trans Nzoia inaitaka serikali kuingilia kati ili kupata suluhu kuhusu mzozo wa shamba la zahanati hiyo, shamba linalodaiwa kunyakuliwa na mtu binafsi.

Wakazi wanalalama kupitia wakati mgumu kupata huduma kwenye zahanati hiyo kufuatia mzozo wa mara kwa mara kati ya uongozi wa zahanati na mmiliki wa shamba ambaye anadaiwa kuzuia upanuzi wa majengo ya zahanati hiyo.

“Baada ya uchunguzi tuligundwa kwa shamba la zahanati limenyakuliwa na mtu binafsi. Hili ndio Zahati inayotumika eneo la ziidi kilomita kumi” asema Chifu.

Madai hayo yamedhibitishwa na naibu chifu wa eneo hilo akieleza kuwa hali hiyo inahitaji hatua ya dharura kwa manufaa ya wakazi.