Hisia mseto zaibuka miongoni mwa wananchi: Bungoma (Video)

0
760

by Christine Musundi

Hisia mseto zaibuka miongoni mwa wananchi huku idadi kubwa ya wanasiasa ikionekana kuunga mkono BBI

Mazishi ya mama Jane Mchebi imeadhimishwa nyumbani kwake Muyenga Kaunti ya Bungoma akiwa mwanachama wa Ford Kenya.

Viongozi kadhaa wamehudhuria hafla hiyo huku Mbunge wa Bumula Mwambu Mabonga akiwaongoza wanasiasa mbalimbali katika nafasi ya kutoa hoja zao za kisiasa.

Vilevile Naibu Gavana Charles Ngome miongoni mwa wanasiasa wengine amewakashfu viongozi wa Ford Kenya kwa kutupia cheche za matusi zilizoibua hisia kati yao na kusababisha vuta nikuvute.

 

Hata hivyo, Seneta wa Kaunti ya Bungoma Moses Wetangula amesuta vikali siasa za ukabila katika vyama.Suala la BBI likiwa kizungumkuti, waliohudhuria mazishi hayo nia kuu ikiwa ni kutaka kujulishwa mengi kuhusiana na mchakato huo ambao kila mwanasiasa anaupigia debe.

 

kando na hayo, suala la kukusanya sahihi halikuachwa nyuma kuzungumziwa na viongozi