Mwanabiashara Namasaka atofautiana na kauli ya waislamu: BBI (video)

0
376

Kauli ya uongozi wa dini islam nchini kumtaka rais Kenyatta kusitisha kampeni za BBI na kuzingatia juhudi za kukabili gonjwa la korona imepngwa vikali na mfanyibiashara mashuhuri mjini Bungoma, Cornelius Namasaka.

Akihutubia wanahabari afisini mwake, Namasaka ameeleza kuwa ripoti ya BBI ina vigezo muhimu vinavyolenga kurejesha hadhi ya taifa, hvyo basi ripoti hiyo haipaswi kupuuzwa.

Kuhusu tetesi za idara ya DCI kurejelea kesi ya baada ya uchaguzi wa 2007, namasaka ameunga mkono hatua hiyo akiwakosoa wanasiasa wanaoonekana kuipinga, hasa wandani wa naibu rais William Ruto.

Aidha, mfanyibiashara huyo amesikitika kuhusu hali tete ya kisiasa inayoshuhudiwa katika taifa jirani la Uganda akinyosha kidole cha lawama kwa uongozi wa jumuia ya Afrika mashariki kwakutotoa muongozo wa kushinikiza demokrasia na haki katika mataifa yanachama.