Marcus Rashford anyakuwa nafasi kwenye orodha ya wachezaji bora

0
557

Imeandikwa na ALPHA DARWIN,

Mchezaji wa klabu ya Manchester United na nchi ya Wingereza Marcus Rashford ameweza kupata nafasi kwenye orodha ya wachezaji weusi wenye roho kama ya malaika baada ya kampeni yake ya kuweza kuwasaidai watoto ambao hawana uwezo wakupata chakula na wanaoishi kwa umasikini.

Rodney Hinds ndiye alianzisha shughuli hii mnamo mwaka wa 2008 ambapo wanaoshiriki huweza kuchaguliwa na kamati ya mabingwa kutoka kwa jamii ya watu weusi na mabingwaa wa michezo duniani.

Ikumbukwe kuwa juhudi za Rashford za kuwatetea watoto wasio weza kupata chakula ziliwemuwezesha pia kupata tuzo la M.B.E . Wachezaji wengine ambao walijiunga na rashford kwenye kikundi hiki cha wachezaji wema ni; wachezaji wa Crystal Palace,Chloe Morgan na Wilfred Zaha,Mchezaji wa Aston Vila Tyrone Mings na Mchezaji wa klabu ya Watford Troy Deeny

Aidha watangazaji wa shirika la utangazaji la skysport Jessics Creighton na Micah Richard pamoja na mtangazaji wa shirika la kibinafsi Charlene pia wamepata nafasi kama Mitandao bora  zaidi kwenye shughuli hii nzima