Juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa kisukari (Video)

0
459
diabetes-testing-POHO:WHO

Wallace wanjala

Naibu Gavana wa kaunti ya trans nzoia Stanely Tarrus ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hiyo na wananchi kwa ujumla kuwajali wangonjwa wa kisukari ili kuwaepusha na makali ya ugonjwa wa Corona.

Madai yake yameungwa mkono na waziri wa afya kwenye kaunti hiyo Clare Wanyama akiwataka wananchi kujitokeza ili kufanyiwa vipimo na kubaini hali yao mapema.

Wawili hao walihutubu kwenye hafla spesheli ya kuwajali wagonjwa wa kisukari kwenye kaunti hiyo huku baadhi ya wagonjwa wakilalama kuhusu gharama ya kusaka dawa ya kudhibiti makali ya ugonjwa huo wakiitaka serikali kuingilia kati.

Aidha, wito umetolewa kwa wagonjwa wa kisukari wenye umri mdogo kutokata tama maishani na badala yake kukumbatia matibabu.