Serikali imetupilia mbali janga la korona na kuipa kipaumbele BBI(video)

0
584

By Christine Musundi,

Janga la korona likiendelea kuzua hofu kwa wakazi wa Sinoko Kaunti ya Bungoma wameikashifu serikali kuu kwa kutoajibika kudhibiti covid-19 ilhali wameipa BBI kipaumbele.

 

Kulingana na kauli ya mkazi wa eneo hilo, wanahofia maisha yao yamo hatarini haswa wakati huu ambapo serikali inashughulikia mchakato wa BBI pasipo kujali afya ya mwananchi.

Vilevile wanabodaboda wa eneo hilo wametoa taswira kamili kwa serikali kwamba hamna haja ya kuunga mswada wa BBI huku wakenya wakizidi kuangamia.

Hata hivyo kulingana na mwenyekiti wa wanabodaboda ameinyoshea serikali kidole cha lawama kwa kutosambaza nakala za BBI mashinani huku akitoa lawama kuwa viongozi wamejitakia nyadhifa wao wenyewe bila kuwapa wanabodaboda nafasi.

Aidha amedokeza kuwa hawana uwezo wa kulipia gharama ya covid-19 hospitalini kwa hivyo wanahitaji kadi za bima ya afya(NHIF) zirejeshwe kwa wananchi wa mashinani.

Kando na uchochole wameiomba serikali kiujumla kushughulikia wananchi mashinani ipasavyo kwani janga la corona linaendelea kunoa makali huku idadi kubwa ikishuhudiwa ya maambukizi na maafa.

Swali ambalo limewabakisha vinywa wazi ni je?Serikali itategua lini kitendawili cha covid-19