Mwanaume na kipaji cha Ususi Mayanja, Bungoma(Video)

0
504
photo by CGN
David Nambafu Sitaka akisuka mteja akiwa Mayanja

By Mercy Wangila

Ususi wa nywele umejulikana kama kazi ya watu wa jinsia ya kike pekee, lakini kauli hiyo imeonekana kukanushwa na baadhi ya vijana, ambapo wengi wao wamedai kutopata ajiri hata baada ya kuhitimu masomoni.

Katika eneo la Mayanja Kaunti ya Bungoma, nimekutana na mwanamume mmoja, raia wa nchi jirani ya Uganda, kijana aliyesomea taaluma ya ualimu na hatimaye kusomea kazi ya ususi baada ya kazi ya ualimu kugonga mwamba.

Aidha, kazi ya ususi ameifanya kwa miaka mitatu sasa, miwili Uganda na mmoja Kenya. Sababu kuu ya kuja kwake na kuifanya kazi ya ususi nchini ni kuwa, thamani ya shilingi ya Kenya ni ya kiwango cha juu ikilinganishwa na ya Uganda. Vilevile amedai kuwa wanawake humu nchini wanapenda kusuka nywele zao.

photo by CGN
David Nambafu Sitaka akisuka mteja akiwa Mayanja

“Napenda kufanya kazi karibu na vituo vya mafuta ambapo wateja wengi hupatikana,”alisema.

“Hata hivyo, msusi huyo amewataka vijana wasio na ajira kujiunga naye kwani cha muno ni kupata fedha za kuyakimu maisha”. Haya ameyasema akiwa anamwelekeza mmoja wa vijana hao jinsi ya kusuka.

Kama kawaida, hakuna kizuri kisichokuwa nakasoro, kijana huyo anapitia changamoto si haba, ambapo amedai kuwa baadhi ya wanaokuja kusukwa huwa hawataki kulipia huduma hiyo.