Ajuza wamiaka80 asaidia mama wajawazito (Video)

0
523
CGN

by Christine Musundi

 Nyanya mwenye miaka 80 kaunti ya busia katika kijiji cha budokomi amejitolea kuwasaidia kina mama wajawazito kulea mimba zao hadi watakapofika kilele cha kujifungua, akishirikiana pamoja na Hospitali ya Mandende kaunti ndogo ya Nambale.

Akiwa nyumbani kwake amehoji kuwa yeye hufanya kazi hiyo wakati wowote anapoitwa au kutembelewa na mteja anayehitaji kuhudumia.wakati huo huo ametaja kuwa angependa wahudumu wa afya kuwaangazia maslahi yao haswaa wakati wa usiku wanaposafiri kwani ni vigumu kumfikisha mama mjazito hospitalini.

Akijivunia utendakazi wake, ameeleza kuwa yeye ni mama ambaye ana ujuzi.Kando na masomo amafanya kazi hiyo kwa muda mrefu . Pia amewahudumia wateja akiwaondolea maumivu huku akiwakanda tumbo na kuhakikisha anajihisi vyema.mama huyo anatabasamu kwa wateja wake wote ishara kwamba hajashuhudia maafa yoyote kwa kazi hiyo.

Aidha amewaomba kina mama wanaotarajia kupata watoto wakati huu wa covid-19 kuhudumiwa hospitalini wakiwa na mkunga aliyehitimu kwenye idara hiyo. Vilevile wahudumu wa afya kujali maslahi yao kama mama mkongwe anayesaidika kina mama kwa kuwapa vifaa maalum vya kisasa hata wanapofanya shughuli hizo nyumbani.