Hamasisho dhidi ya Corona mpakani Busia Teso Kusini

0
423
Trucks in Malaba border, Photo courtesy Nation.Africa

By Christine Musundi

Wiki chache zilizopita wakenya wengi wameonekana kukaidi maagizo yakuzuia maambukizi zaidi ya Corona.Wengi wao wametangamana kwa kutozingatia kanuni zilizowekwa na wizara ya afya. katika Kaunti ya Busia Teso Kusini kata ndogo ya Kotur,wakazi wanajaribu kadri ya uwezo wao kudhibiti maambukizi hayo.

Trucks in Malaba border, Photo courtesy Nation.Africa

Hata hivyo Dennis Irono chifu wa maeneo hayo, ameanzisha vikundi mbalimbali miongoni mwao wanabodaboda ili kuwahamasisha wanakijiji  dhidi ya kujikinga na janga la Corona.vilevile mwenye mwenyekiti wa wanabodaboda wicliffe Angate amemwunga mkono chifu eneo hilo kuwa ni sharti dereva wa pikipiki kuhakikisha amebeba abiria mmoja na sio zaidi huku abiria huyo akiwa amevalia barakoa.

“kando na hayo suala la BBI halijaachwa nyuma kuzungumziwa,” alisema Rono .  Aidha,wanabodaboda wamenyoshea  kidole cha lawama serikali kuu kwa kutowajibika kusambaza Nakala za BBI mashinani kwa mwananchi wa kawaida.

Mwenyekiti wa wanabodaboda ambaye pia yuko miongoni mwa vikundi vinavyotumika kuhamasisha umma dhidi ya Covid-19, amekuwa na haya ya kusema, “ni sharti wanaoabiri pikipiki wanawe mikono ndiposa waendelee na safari yao.”