Wanafunzi wa Shule ya Wasichana Kibabii wako tayari kupata masomo

0
586
21CA
Photo courtesy 21CA 2019, Kibabii-Girls-Boarding-School

By Mercy Wangila

“Masomo, ni ufunguo wa maisha “, wahenga walisema, naukimwelisha mtoto wa kike, bila shaka umeelimisha jamii. Leo hii nimeangazia hali halisi katika Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maria ya Malazi ya Kibabii.

Takriban miezi saba hivi, visa vya mimba za mapema vimeshuhudiwa kuongeka miongoni mwa wanafunzi wa kike, ambao wamedai kutoweza kumudu visodo vya kutumia wakati wa hedhi.

Katika shule hiyo ,mambo ni tofauti, “wanafunzi wanakila sababu ya kutabasamu, kisa na maana , visodo vya kila aina vipo kwa ajili yao, wakiwa shuleni na hata nyumbani’’, alisema mwalimu mkuu.

“shule zilipofunguliwa kwa muhula wa pili, wanafunzi wa Gredi ya nne na Darasa la Nane walijitokeza isipokuwa kwa wawili, waliowasilisha ujumbe kwa Mwalimu Mkuu.. Kwa wanafunzi waliorejea, hakuna aliyebeba ujauzito jinsi inavyoshuhudiwa kwa sasa,”Mwalimu Mkuu aliendelea kueleza.

Nakala za Mfumo Mpya wa CBC kwa wanafunzi wa Gredi ya Nne vilikuwepo kwa wingi, kiasi cha kutosha kila mmoja wao, tofauti na ilivyokuwa awali,” Mkuu wa shule hiyo aliongezea.