Hali tete,Ukosefu wa walimu na madarasa

0
392
Courtesy of Citizen tv kenya

By Mercy Wangila

Munamo Machi mwaka huu, covid-19 ilizuka nchini Kenya.Shughuli nyingi zilisitishwa zikiwemo za masomo. Wanafunzi wakalazimika kurudi nyumbani njia mojawapo wa kudhibiti maambukizi zaidi.Sheria na masharti ziliwekwa kufuatwa na kila mwananchi.
Takriban siku 180 baadaye , wanafunzi wa darasa la 8 na gredi ya 4 waliamrishwa kurejea shuleni kwendelea na masomo yao, wakuu wa shule wakawa na hofu ya jinsi watakavyoendesha sheria hizo.
je, hawa
shule ya upili ya friends bukananachi, ni shule iliyoanzishwa mwaka2014 kwenye ardhi isiyozidi ekari 1.cha kusikitisha ni kwamba shule hiyo ina majengo mawili pekee. jengo la kwanza limegawanywa maranne yaani majilisi , afisi ya mwalimu mkuu, afisi ya karni, na kadhalika. la pili ndipo sasa mahali rasmi pa wanafnzi kusomea, limegawanywa kwenye madarasa manne yaani kidato cha 1,2,3 na 4.jmla wanafunzi ni 185. wanafunzi 185 wakigawanywa na madarasa yaliyopo ina maana kuwa kila darasa linabeba wanafunzi 45 na hata zaidi.swali ni je, wanafunzi wengine wakirejea itakuwaje?

“Madarasa kwa sasa yanatosha wanafunzi waliopo ila naomba madarasa zaidi yaongezwe,” alisema mwalimu mkuu.
“Isitoshe twaiji idadi ya walimu kuongezeka ambapokwa sasa tuna jumla ya walimu10, sita wa TSC na wanne wa PTA”,aliongezea.

“Kama ilivyoada, wanafunzi kwenye shule za upili kula chamcha shuleni,chakula hicho hulipiwa na wazazi, ila wengi wao wamepuuza, kisa na maana, waziri wa elimu aliarisha wanafunzi hao kurudi shuleni hata pasipo kukamilisha karo,” alisemamkuu washule hiyo.