Masaibu ya wakulima wa miwa

0
481
Photo courtesy;FarmLINK kenya

By Mercy Wangila

Wakulima wa miwa eneo la Ranje katika Kaunti ya Bungoma, wamelalamikia changamoto wanazopitia tangu waanze kupanda upanzi wa miwa hiyo.

Kwa mujibu wa mojawapo wa wakulima hao,Kampuni ya nzoia imekuwa ikiwalipa vizuri mwanzoni ,ila ilianza kufifia baada ya miaka kadhaa, hali iliyowalazimu wengine wao kutafuta soko kwenye kampuni zingine.

Upanzi wa miwa umekuwa wa manufaa kwa wakulima hao ambao wamedai kuwa imewsadia pakubwa katika kuelimisha wanao, kununua mashamba miongoni mwa mengine, ila sasa wengi wao wamelazimika kuuza mifugo hata mashamba ili kukimu mahitaji hayo.

Wakati huo huo ,wanafunzi katika eneo hilo ambao kwa sasa wamejitosa katika shughuli za hapa na pale ili kupata fedha za kukimu mahitaji yao, wametoa wito kwa wizara ya elimu kufanya kila iwezalo ili waweze kurejea shuleni kwendelea na masomo.

Hata hivyo, wakulima hao wamependekeza kuruhusiwa kuuza miwa zao kwenye soko huru iwapo kampuni itakosa kuwajibika kikamilifu.Swali ni je, kitendawili hiki kitageliwa lini?

Photo courtesy;FarmLINK kenya