Wana ESTEP kuugeuza uwanja wa ndege kuwa uwanja wa mchezo wa kandanda

0
537

Na, Presenter Darwin

Kikundi cha kuhifadhi talanta hasaa mchezo wa kandanda kinachofahamika kama ESTEP ambacho kinapatikana katika kaunti ya Bungoma,kimeweza kuwaomba wahisani wao ambao ni serikali ya kaunti hio kuweza kuwasaidia vifaa vya kutumia kwenye mchezo huo ikiwemo:Mipira,sare na vifaa vingine vingi ambavyo vitawawezesha watoto hao ambao wapo chini ya miaka kumi na mitano kuzikuza talanta zao.

Aidha akizungumza na jarida hili kocha wa timu hiyo Micheal Ariga aliiomba pia serikali ya kaunti kuharakisha ujenzi wa uwanja wa michezo wa Bungoma ili kuwapa nafasi nzuri ya mazoezi ikizingatiwa kuwa wanatumia uwanja wa ndege.

Mmoja wa wachezaji wa timu hio alielezea jinsi mazoezi wanayoyafanya kila siku kuanzia mida ya saa tatu hadi saa kumi yamemuwezesha kuepuka vikundi vibaya na pia kuikuza talanta yake,licha yakwamba mtoto anaitaji kulipia ada ya shilingi elfu mbili ili kujiunga na timu hio Wisdom aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto wao kujumuika nao kwani aliitaja kama sehemu bora kwa wote walio na talanta ya kuucheza mchezo wa kandanda na walio na ndoto ya kufika mbali.